Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 11:39

Mfumuko wa bei nchini Zimbabwe wafikia kiwango cha zaidi ya asilimia 130


Mwanaume aonekana nyuma ya gari ya mazigo ambayo imewasili mjini Harare kutoka Afrika Kusini, ikibeba chakula, March 22, 2022. Picha ya AFP
Mwanaume aonekana nyuma ya gari ya mazigo ambayo imewasili mjini Harare kutoka Afrika Kusini, ikibeba chakula, March 22, 2022. Picha ya AFP

Kiwango cha mfumuko wa bei nchini Zimbabwe kimeongezeka hadi asilimia 131.7 mwezi huu wa Mei, idara ya takwimu imesema Jumatatu, huku athari za vita vya Ukraine zikiathiri uchumi ambao tayari ulikuwa umeathirika.

Mfumuko wa bei ulifikia kiwango cha zaidi ya asili mia moja kwa mara ya kwanza tangu mwezi Juni mwaka jana huku bei ya mafuta ya kupikia na mkate ikifikia viwango vya juu kutokana na uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine.

Wiki iliyopita, serikali ilijaribu kupunguza bei kwa kuondoa ushuru kwenye bidhaa muhimu zinazoagizwa nje kama mafuta ya kupikia, mchele na unga.

Mfumuko wa bei ulikuwa tayari asilimia 96.4 mwezi Aprili, idara ya kitaifa ya takwimu imesema katika taarifa.

Uhaba wa fedha za kigeni ulipelekea makampuni ya ndani ya nchi kusumbuka kununua vifaa kutoka nje ili kuzalisha bidhaa nchini Zimbabwe.

XS
SM
MD
LG