Wauguzi nchini humo wanalipwa dola18,000 za Zimbabwe ambazo ni sawa na dola 55 za kimarekani kulingana na soko la ubadilishanaji la sasa. Mshahara wa walimu unasemekana kuanzia dola 75 kwa mwezi. Wafanyakazi wa afya walikusanyika nje ya ofizi za bodi ya kitaifa ya afya, ilioko kwenye mojawapo ya hospitali kubwa zaidi nchini humo.
Askari wa kuzima ghasia waliitwa karibu na eneo hilo wakati wagonjwa hospitalini wakiachwa bila huduma zozote. Kiongozi wa shirika la wauguzi la Zimbabwe Enock Dongo amesema kwamba bodi ya afya pamoja na wizara ya afya wamekataa kusikiliza kilio chao. Wiki iliopita serikali ilisema kwamba ingeongeza maradufu mishahara ya wafanyakazi wote wa serikali, lakini Dongo amesema kwamba kufikia sasa hakuna hatua yoyote rasmi iliyopigwa.