Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 11:41

Zimbabwe: Wafanyabiashara waonya juu ya athari za hatua ya kusitisha ukopeshaji kwenye benki


Wateja wakisubiri kwenye foleni kuchukua pesa kwenye benki mjini Harare, baada ya Benki kuu ya Zimbabwe kutoa noti mpya, Novemba 12, 2019. Picha ya AP
Wateja wakisubiri kwenye foleni kuchukua pesa kwenye benki mjini Harare, baada ya Benki kuu ya Zimbabwe kutoa noti mpya, Novemba 12, 2019. Picha ya AP

Hatua ya Zimbabwe ya kusitisha ukopeshaji wa benki itakuwa na matokeo mabaya, itaunda mfumo sambamba wa benki na kukwamisha juhudi za kuboresha uchumi unaodorora, wakuu wa sekta ya biashara nchini humo wamesema Jumatatu.

Rais Emmerson Mnangagwa Jumamosi aliamuru benki kusitisha kukopesha kama sehemu ya hatua kadhaa alisema zinalenga kuweka sawa uchumi usiendelee kudorora.

Mnangagwa alisema hatua hiyo itasitisha kuporomoka kwa dola ya Zimbabwe na kuzuia ukuaji wa soko sambamba ambapo dola ya nchi hiyo ilikuwa ikibadilishwa kwa karibu dola 400 za Marekani, ikiwa mara mbili zaidi ya kiwango rasmi cha wiki iliyopita.

“Serikali imesitisha huduma za benki lakini benki bado ziko imara,” chama cha biashara cha Zimbabwe kimesema katika taarifa.

“Hii inahalalisha mfumo sambamba wa benki na viwango vya juu vya riba na hakuna mwekezaji atakayevutiwa na uchumi kama huo ambapo ukopeshaji unaweza kusimamishwa gafla,” chama hicho kimeongeza.

Chama hicho kimesema serikali ilipuuza ushauri kutoka kwa sekta ya wafanyabiashara kuhusu namna ya kufufua uchumi.

Uchumi wa Zimbabwe umekuwa ukidorora kwa zaidi ya mwongo mmoja.

XS
SM
MD
LG