Dangarembga na mshtakiwa mwenzake Julie Barnes, ambaye pia alipatikana na hatia, walikuwa wameshtakiwa kwa kushiriki katika mkutano wa hadhara kwa nia ya kuchochea ghasia za umma wakati wa kuvunja itifaki za COVID-19, baada ya kufanya maandamano mnamo Julai 2020.
Wawili hao walitozwa faini ya dola 70,000 za Zimbabwe na kupokea hukumu iliyosimamishwa, mradi hawatatenda kosa kama hilo katika siku zijazo.
Mkosoaji mkali wa serikali ya Rais Emmerson Mnangagwa ambaye amekuwa akipigana kwa miaka mingi dhidi ya ufisadi na kutaka mageuzi, Dangarembga alikuwa ameshikilia wakati wa kesi hiyo kwamba Wazimbabwe wana haki ya kuandamana.
Wawili hao walinuia kuchochea ghasia na washtakiwa wamepatikana na hatia kama walivyoshtakiwa,hakimu wa Harare Barbara Mateko alisema.