Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 09:46

Umoja wa Afrika wataka vikwazo vya kimataifa kuondolewa dhidi ya Zimbabwe


FILE PHOTO: EU/AU summit in Brussels
FILE PHOTO: EU/AU summit in Brussels

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Macky Sall wa Senegal ametoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Zimbabwe na kuongezwa kwa huduma za dharura kwa nchi za Afrika.

Akifungua mkutano maalum wa viongozi wa Afrika mjini Malabo, Equatorial Guinea kiongozi huyo alitangaza msaada mdogo wa dola milioni 3 kutoka nchi yake kwa ajili ya huduma za dharura barani afrika.
Mkutano huo wa viongozi wa siku mbili utajadili juu ya mzozo wa kibinadamu, ugaidi, na mapinduzi ya kijeshi katika bara hilo. Karibu viongozi 20 wa nchi za kiafrika pamoja na wafadhili wanakutana kwa mkutano wa kwanza maalum wa nchi za Afrika kuchangisha fedha kwa ajili ya huduma za dharura.
Mwenyekiti wa kamisheni ya Afrika Moussa Faki Mahamat amesema kwamba karibu waafrika milioni 113 wanahitaji huduma ya haraka ya msaadawa dharuramwaka huu ikiwa ni pamoja na watu milioni 48 ambao ni wakimbizi, wanaotafuta hifadhi na walokoseshwa makazi ndani ya nchi zao.
Mkutano wa pili wa viongozi wa Afrika hapo kesho, utakabiliana na tatizo la ugaidi na mapinduzi wakati wapiganaji wenye itikadi kali wakizunsha matatizo huko Libya, Msumbiji, Somalia na Kanda ya Sahel.

XS
SM
MD
LG