Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:41

Watu 30 wafariki katika ajali ya boti DRC


Wakazi wa Goma wakiondoka kwa boti baada ya kulazimishwa kufanya hivyo Mei 27, 2021.
Wakazi wa Goma wakiondoka kwa boti baada ya kulazimishwa kufanya hivyo Mei 27, 2021.

Takriban watu 30 wamekufa maji na 167 hawajulikani walipo baada ya boti kupinduka kwenye mto Kongo Ijumaa jioni kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, waziri mmoja wa jimbo aliambia Reuters  Jumapili.

Didier Mbula, waziri wa afya wa jimbo la Equateur, alisema kuwa watu 189 wameokolewa na kwamba shughuli za kuwatafuta manusura wengine zinaendelea.

“Kulingana na idadi tuliyo nayo hadi sasa kama serikali ya jimbo, maiti 30 zimeopolewa, na watu 167 hawajapatikana,” alisema Mbula.

Ajali mbaya za boti hutokea mara kwa mara katika mito na maziwa ya Kongo, ambapo boti mara nyingi hupakiwa kupita kiAsi.

Nchi hiyo ina barabara chache za lami katika eneo lake kubwa lenye misitu, na kusafiri kupitia mito ni jambo la kawaida.

Boti hiyo iliyotengenezwa kienyeji ambayo ilipinduka karibu na mji wa Mbandaka ilikuwa imejaa kupita kiasi, ikiwa imebeba zaidi ya watu 300, na ilikuwa ikisafiri usiku, Mbula alisema.

"Tunafikiri kwamba idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka kwa sababu tumeondoa maiti ya 30," alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG