Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 00:55

Zaidi ya watu 20 wafariki kutokana na ajali ya feri Nigeria


Picha ya ferry mjini Lagos, Nigeria. Picha ya maktaba.
Picha ya ferry mjini Lagos, Nigeria. Picha ya maktaba.

Takriban watu 26 wamekufa na wengine hawajulikani walipo baada ya ferry kuzama kasakazini mwa eneo la katikati mwa Nigeria Jumapili, maafisa wa kieneo wamesema , ikiwa ajali ya pili kubwa kufanyika kwenye eneo hilo ndani ya miezi mitatu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Bogoli Ibrahim, msemaji wa gavana wa jimbo la Niger amesema kwamba ferry hiyo ilikuwa imebeba zaidi ya watu 100 wakiwemo wanawake na watoto kwenye eneo la Mokwa.

Waliokuwa kwenye ferry hiyo walikuwa wakivuka bwawa kubwa wakielekea kwenye mashamba yao, ameongeza Ibrahim. Watu 26, wengi wao wakiwa watoto na wanawake wamedhibitishwa kufa, huku wengine zaidi ya 30 wakiokolewa.

Shughuli za uokozi zinaendelea zikiongozwa na Idara ya dharura ya jimbo la Niger, ikishirikisha polisi wa majini pamoja na wapiga mbizi. Mwezi Julai, zaidi ya watu 100 walikufa baada ya boti iliyokuwa imejaa kupita kiasi kuzama kwenye eneo lililopo ndani katika jimbo hilo la Niger, ikiwa ajali mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miaka ya karibuni.

Forum

XS
SM
MD
LG