Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:47

Wanajeshi 6 wa Afrika Kusini wafariki katika ajali ya moto


Wanajeshi wa Afrika Kusini
Wanajeshi wa Afrika Kusini

Wanajeshi sita wa Afrika Kusini walifariki baada ya moto kuzuka katika kituo cha mafunzo cha jeshi kaskazini mashariki mwa nchi, jeshi limesema Jumamosi.

Jeshi la Afrika Kusini limesema moto huo uliteketeza moja ya vituo vyake vya mazoezi siku ya Ijumaa mchana.

Moto ulielezwa kusambaa hadi kwenye eneo la kambi ukianzia kwenye mgodi wa karibu na kambi ya kijeshi.

“Iliripotiwa kuwa wanajeshi sita walipoteza maisha wakati wa tukio hilo,” jeshi limesema katika taarifa.

Wanajeshi wengine watatu walijeruhiwa vibaya na walipelekwa kwenye hospitali iliyo karibu.

Wanajeshi hao walikuwa wanajiandaa kwa mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka.

Forum

XS
SM
MD
LG