Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 07:32

Rais Kais wa Tunisia akata msaada wa EU kusaidia kukabiliana na uhamiaji


Rais Kais Saied akizungumza baada ya serikali mpya kula kiapu, Feb, 27, 2020.
Rais Kais Saied akizungumza baada ya serikali mpya kula kiapu, Feb, 27, 2020.

Rais Kais Saied wa Tunisia amekata msaada wa fedha ulotangazwa na Umoja wa Ulaya, EU mwezi uliyopita, akisema idadi ni ndogo na ina kwenda kinyume na mkataba ulotiwa saini miezi mitatu iliyopita.

Uwamuzi wa Saed unaweza kuhujumu mkataba huo wa ushirikiano wa usalama ulofikiwa Julai, ambao ulihusisha pamoja na mambo mengine, hatua za kupambana na ulanguzi wa binadamu na kufunga zaidi mipaka yake, kufuatia kuongezeka sana safari za boti kuelekea Ulaya kutoka taifa hilo la Afrika ya Kaskazini.

Kamisheni ya EU ilitangaza mwezi uliyopita kwamba itatoa msaada wenye thamani ya dola milioni 133 kwa Tunisia, kama sehemu ya kukabiliana na uhamiaji haramu kutoka Afrika kuelekea Ulaya.

Said amesema, Tunisia inapinga kile EU imetangaza sio kwa sababu idadi ni ndogo, lakini kwa sababu pendekezo linakinzana na makubaliano ya muelewano iliyotiwa saini mwezi Julai.

Makubaliano ya Julai yaliahidi msaada wa Euro bilioni moja kwa Tunisia, ili kuisadia kukabilaina na hali ngumu ya kiuchumi, kuokowa hazina ya taifa na kukabiliana na mzozo wa uhamiaji.

Forum

XS
SM
MD
LG