Moja ya boti hizo ilikuwa imebeba wahamiaji 280, idara ya dharura ya visiwa hivyo imesema kwenye mtandao wa X uliojulikana awali kama Twitter.
Shirika la habari la serikali EFE limesema ilikuwa ni idadi kubwa ya wahamiaji ndani ya boti moja tangu wasafirishaji haramu wa binadamu walipoanza kutumia mara kwa mara njia ya kisiwa cha Canary mwaka 1994.
Mratibu wa shirika la Mslaba Mwekundu la Uhispania Antonio Rodriguez Verona ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa hajaona watu wengi kiasi hicho ndani ya boti moja tangu mwaka 2008, wakati wahamiaji 234 walipofika sehemu hiyo wakiwa ndani ya boti moja.
Mamia ya wahamiaji wengine walizuiliwa wakijaribu kufika kwenye visiwa vingine vilivyoko kaskazini magharibi mwa pwani ya Afrika, mahali pengine kwenye ardhi ya Uhispania katika siku za hivi karibuni.
Forum