Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:37

Watu 21 wafariki katika ajali ya basi lililokuwa limebeba watalii katika mji wa Italy wa Venice


Maafisa wa polisi wakifanya ulinzi nje ya kambi ya kitalii ya Hu, baada ya basi la abiria kufanya ajali katika mji wa Mestre, karibu na mji wa Italy wa Venice, Oktoba 4, 2023.
Maafisa wa polisi wakifanya ulinzi nje ya kambi ya kitalii ya Hu, baada ya basi la abiria kufanya ajali katika mji wa Mestre, karibu na mji wa Italy wa Venice, Oktoba 4, 2023.

Basi lililokuwa limebeba watu kadhaa lilitumbukia kina cha mita 15 kutoka barabara ya juu katika mji wa Venice nchini Italy, na kusababisha ajali mbaya iliyoua watu 21 na kujeruhi wengine 15, wengi wao wakiwa watalii wa kigeni waliokuwa wakirejea kwenye kambi iliyo karibu.

Miongoni mwa waliofariki katika ajali hiyo ya Jumanne usiku ni Waukraine watano, raia mmoja wa Ujerumani na dereva wa basi hilo, kulingana na wilaya ya Venice.

Wawili kati ya waliofariki ni watoto, mkuu wa wilaya ya Venice Michele Di Bari amesema, akiongeza kuwa waathirika wengi katika ajali hiyo walikuwa vijana.

Watu tisa akiwemo mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu kutoka Ukraine walikuwa katika hali mbaya, maafisa wa hospitali wamesema Jumatano asubuhi.

Basi hilo lilikuwa limebeba watalii wa kigeni kutoka mji wa Venice kuelekea kambi ya kitalii ya Hu Jumanne jioni wakati basi lilipoanguka kutoka barabara ya juu karibu na njia ya reli katika mtaa wa Mestre na kushika moto.

Forum

XS
SM
MD
LG