Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:39

Watetezi wa wanawake wasema safari ya kutibu msongo wa mawazo ni ndefu


Tatizo la afya ya akili kwa vijana.
Tatizo la afya ya akili kwa vijana.

Wanawake wengi wanapitia msongo wa mawazo baada ya kujifungua, wengi wao wakijikuta katika hali ngumu zaidi kwa kukosa msaada wa mapema.

Watetezi wa wanawake na hasa wa Afya ya akili wanasema safari ya kutibu msongo wa mawazo ni ndefu na inahitaji wanawake zaidi kuzungumzia matatizo yao mapema.

Msongo wa mawazo baada ya kujifungua ni suala zito ambalo wanawake wengi hasa vijana hukabiliana nalo, lakini mara nyingi wengi huona aibu kulizungumzia. Zulfa Njenga anasema sio rahisi ikiwa ndio mara ya kwanza kwa mama kujifungua ilhali hana wa kumwelekeza.

Alipata mfadhaiko zaidi baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji. Hakuwa na maziwa ya kumpa mwanawe na kwa kuwa alikuwa mama wa mara ya kwanza, alilia sana.

Tatizo la afya ya akili kwa vijana.
Tatizo la afya ya akili kwa vijana.

Alibahatika kuwa na familia yake karibu naye ili kumsaidia katika kipindi hiki kigumu

Msongo wa mawazo baada ya Kujifungua huathiri zaidi ya asilimia 10 ya wanawake duniani kote. Ingawa changamoto hii ya afya ya wanawake bado haijatambuliwa nchini Kenya, serikali imeweka mifumo ambayo inaruhusu wanawake kutafuta msaada mara moja.

Judy kihumba mtetezi wa afya ya akili ya akina mama ambao wanachangamoto ya kusikia, anasema tatizo hili mara nyingi huwapata wanawake ambao ni viziwi .

Ni kupitia masaibu ya wanawake hasa waliona changamoto ya kusikia , hapo ndipo Judy Kihumba akaanzisha mchakato wa kuwasaidia kimama waliojifungua kukabili suala la msongo wa mawazo hasa wanawake Viziwi.

Anasisistiza ni vyema wanawake kujuliana hali kabla ya kujifungua na baada. Hatua anasema itasaidia wanawake pakumbwa katika kujieleza yanayo wasibu

Nchini Kenya, takriban msichana 1 kati ya 5 wenye umri wa miaka 16-19 ni wajawazito au tayari wamekuwa mama. Ingawa wanawake hupata changamoto kama vile mfadhaiko, wasiwasi, na mfadhaiko kutokana na ujauzito wao, utafiti unaonyesha kwamba wao pia wanakabiliwa na vikwazo vya afya kabla ya kujifungua.

Kenya ina wahudumu wa afya ya akili wasiopungua 500 wanaohudumia watu zaidi ya milioni 50. Sasa, mipango ya kijamii inakuzwa ili kujaza pengo hili kwa wasichana wajawazito na wazazi.

Hubbah Abdi, Mwandishi wa VOA Nairobi

Forum

XS
SM
MD
LG