Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:35

Ulimwengu waadhimisha siku ya afya ya akili


Mgonjwa wa kiakili kwenye kituo cha afya nchini Yemen kwenye picha ya maktaba
Mgonjwa wa kiakili kwenye kituo cha afya nchini Yemen kwenye picha ya maktaba

 Jumatatu ni siku ya kimataifa ya afya ya akili, ambapo shirika la afya duniani WHO, limezindua kampeni ya uhamasishaji kwenye maeneo yenye idadi kubwa ya vifo kutokana na kujiua.

Shirika hilo limesema kwamba janga la Covid-19 lilisababisha janga la kimataifa la afya ya akili, ambalo limepelekea msongo wa mawazo kwa mamilioni ya watu kote ulimwenguni. Takwimu kutoa WHO zinaonyesa viwango vya wasiwasi pamoja na msongo wa mawazo, viliongezeka kwa zaidi ya asilimia 25 katika mwaka wa kwanza wa janga hilo.

Wakati huo huo huduma za afya ya akili zilitatizika na kwa hivyo kuwa vigumu kwa waathirika wengi kupata msaada. Tatizo hilo linasemekana kuwa kubwa zaidi barani Afrika, ambako kuna mtaalam mmoja wa kiakili kwa kila watu nusu milioni, ikiwa chini ya mara 100 ya pendekezo la WHO. WHO limesema kwamba watu 11 katka kila watu laki moja barani Afrika hujitoa uhai, ikilinganishwa na watu 9 kwa kila laki moja kwenye maeneo mengine ya ulimwengu.

Bara hilo linasemekana kuwa na mataifa 6 kati ya 10 yenye idadi kubwa zaidi ya watu wanaojitoa uhai kote duniani. Mkurugenzi wa WHO tawi la Afrika Matshidiso Moeti amesema kwamba uwekezaji wa kutosha unahitajika ili kukabiliana na tatizo hilo barani Afrika.

XS
SM
MD
LG