Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:14

WHO yataka nchi za Afrika zichukue hatua kudhibiti ongezeko kubwa la watu kujiua


Shirika la Afya Duniani (WHO) Switzerland.
Shirika la Afya Duniani (WHO) Switzerland.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema Afrika inahitaji kukabiliana na kiwango cha juu  cha watu kujiua lakini bado  kwa kiasi kikubwa  haitambuliwi na aghlabu kunyanyapaliwa.

Nchi sita kati ya kumi zenye idadi kubwa kabisa ya watu kujiua duniani ziko Afrika, na kiwango cha kujiua katika bara hilo ni zaidi ya moja ya tano ikilinganishwa na maeneo mengine, WHO ilisema wiki hii.

“Takriban watu 11 kati ya 100,000 kila mwaka wanafariki kwa kujiua katika eneo la Afrika, ikiwa kiwango cha juu kuliko wastani wa kimataifa wa 9 kwa kila watu 100,000,” tawi la shirika hilo Afrika lilisema.

Vifo vya kujinyonga au kunywa sumu za madawa ya kuua wadudu ni vitendo ambavyo vinaongoza katika orodha.

Shirika hilo limeanzisha uhamasishaji kuongeza uwelewa wa tatizo hili kabla ya Siku ya Kimataifa ya Afya ya Akili inayoadhimishwa Oktoba 10.

“Kujiua ni moja ya tatizo kuu la afya ya umma na kila kifo kutokana na kujiua ni janga. Bahati mbaya njia za kuzuia kujiua ni nadra kupewa kipaumbele katika programu za kitaifa za afya,” alisema mkurugenzi wa kanda Matshidisco Moeti.

Unyanyapaa ni tatizo kuu, kama ilivyo ukosefu wa ufadhili, WHO ilisema.

Afrika ina wastani wa mtaalam mmoja wa magonjwa ya akili kwa kila watu 500,000 – kiwango ambacho kwa asilimia 100 kiko chini na mapendekezo ya WHO – na kuna ukosefu wa matabibu ni kitu kinachotisha katika nchi ambazo zimepitia mizozo.

Matumizi katika afya ya akili Afrika yako chini ya senti 50 kwa mtu, chini ya robo ya mapendekezo ya UN la robo tatu.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG