Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:24

Polisi aua mke wake na watu wengine 5 Kenya


Afisa wa polisi ameuawa watu sita akiwemo mke wake kabla ya kujiua kwa risasi katika mji wa Kabete karibu na mji mkuu wa Nairobi nchini Kenya.

Majirani wamesema kwamba walisikia milio ya risasi mapema jumanne kutoka kwa nyumba ya afisa huyo kwa jina Benson Imbasi.

Baada ya kumuua mke wake, afisa huyo alitoka nyumbani na kupiga risasi watu wengine saba. Watu watano walifariki na wengine wawili kujeruhiwa.

Waliojeruhiwa wanapokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya kitaifa.

Imbasi alijipiga risasi shingoni na kufariki papo hapo.

Kulizuka ghasia kwenye mtaa tukio lilitokea na watu walokua na hasira walipora mali kutoka maduka na kufunga barabara kwa kutia moto matayri.

Polisi wamesema kwamba afisa huyo alitumia bunduki aina ya AK47.

Wanaumme watatu na mwendesha piki piki maarufu boda boda ni miongoni mwa waliouawa.

Polisi wanafanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

XS
SM
MD
LG