Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 08:33

Binti wa miaka 8 apokelewa katika utawa India, yazua mjadala juu ya haki za mtoto


FILE - Mamia ya Watawa wa Jain, kikundi cha Madhehebu ya Wahindu, wanashiriki katika ibada ya siku ya 27 huko Ahmadabad , India Alhamisi Jan 31, 2002.
FILE - Mamia ya Watawa wa Jain, kikundi cha Madhehebu ya Wahindu, wanashiriki katika ibada ya siku ya 27 huko Ahmadabad , India Alhamisi Jan 31, 2002.

Katika picha iliyobandikwa  kwenye ukarasa wa Instagram ikiwa na karibu wafuasi 15,000, msichana mdogo anaonekana akiwa na tabasamu lenye bashasha, amekunja mikono yake kama ishara ya salamu ya utamaduni wa Kihindi.

Amekaa kwenye kiti cha enzi kilichopambwa na maua ya waridi. Akiwa amevaa mavazi ya rangi ya pinki isiyokoza, mapambo ya almasi na taji, anaonekana kama binti wa familia yoyote kitajiri ya Kihindi - akifurahia sherehe ya siku ya kuzaliwa yenye mandhari kama pengine mtoto wa malkia wa Disney.

Maelezo ya picha ya Januari 17, hata hivyo yanaeleza habari tofauti "Antim Vidai Samaroh" - Sherehe ya Mwisho ya Kuagwa.

Siku iliyofuata msichana huyo mwenye umri wa miaka minane Devanshi Sanghvi aliacha nguo zake zenye mchanganyiko wa rangi na maisha ya duniani ya mrithi wa Sanghvi and Sons, biashara ya almasi yenye thamani ya mamilioni ya dola, yenye ofisi zake katika jiji la India la Surat huko Gujarat. .

Katika sherehe zilizopewa jina la "Divya Diksha Danam" au The Divine Brilliance Initiation Donation – pia zimeorodheshwa kwenye ukurasa wa Instagram, Devanshi alikuwa amevaa juba refu jeupe, akiwa bado anatabasamu akingojea kupigwa picha. Ilikuwa kama kwamba hajui kabisa ni nini kinachoendelea: sasa angeishi kama mtawa, kula tu kile anachopokea kama sadaka, kuepuka kutumia teknolojia ya aina yoyote , sio kuoga na hata kuacha na mahusiano yake ya kawaida.

Devanshi anatokea katika familia inayofuata dini ya Jainism, moja ya dini kongwe zaidi duniani – asili yake India.

Ikiwa na wafuasi wapatao milioni 4.5 kote ulimwenguni, kuyasusa maisha ya kidunia siyo jambo geni miongoni mwa Wajaini. Kuwa mtawa mwenye umri wa miaka minane haijawahi kusikika.

Wakiwa wamejihami na picha nyingi na taswira, zilidai kuwa watoto walioingia katika utawa na upadri watakuwa na fursa ya lishe nzuri, elimu ya taaluma, huduma za afya na washauri.

Walezi wa Devanshi wamechunguzwa na wanaharakati kadhaa wa haki za watoto na wataalamu wa afya ya akili.

XS
SM
MD
LG