Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:27

India yaunga mkono juhudi za amani, Modi aitikia wito wa Zelenskyy


Waziri Mkuu wa India Narendra Modi
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ameelezea uungaji mkono wake kwa juhudi za amani nchini Ukraine wakati wa mazungumzo ya simu aliyofanya na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ambapo kiongozi huyo wa Ukraine alitaka msaada wa India katika kutekeleza “mpango huo wa amani.”

“Nilizungumza kwa simu na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na kumtakia mafanikio kwa urais wa G20,” Zelenskyy aliandika katika Twitter Jumatatu. Ilikuwa katika jukwaa hili nilipotangaza mpango wa amani na sasa nategemea ushiriki wa India katika utekelezaji wake.”

India ilichukua urais unaozunguka katika Kikundi cha nchi 20 zenye uchumi mkubwa duniani kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Desemba 1.

Katika hotuba yake kwa G20 kwa njia ya mtandao huko Indonesia mwezi uliopita, Zelenskyy alikitaka kikundi hicho kufuata mpango wa nukta kumi wa amani kwa kuyataka majeshi ya Russia kuondoka Ukraine na kurejesha heshima ya mipaka yake. Alisema wakati huo kuwa “hivi sasa” ndio wakati muafaka kumaliza vita hivyo.

Taarifa kutoka serikali ya India kuhusu mazungumzo ya simu na Zelenskyy Jumatatu jioni ilisema kuwa Modi “anahimiza kwa nguvu zote wito wake wa kusitisha haraka mapigano” na kuongeza kuwa pande zote zirejee katika majadiliano na diplomasia ili kutafuta suluhu ya kudumu kwa tofauti zao.

Taarifa hiyo ilisema kuwa waziri mkuu wa India alielezea uungaji mkono wa nchi yake kwa juhudi zozote za amani, na kumhakikishia Zelenskyy juu ya nia ya dhati ya India kuendelea kutoa misaada ya kibinadamu kwa raia walioathiriwa na vita.

Taarifa hiyo pia ilisema kuwa “Waziri Mkuu alieleza vipaumbele vikuu vya urais wa India katika G20, ikiwemo kuwapa sauti nchi zinazoendelea juu ya wasiwasi wao kwa masuala kama chakula na usalama wa nishati.”

Mazungumzo ya simu kati ya viongozi wa India na Ukraine yamekuja siku kumi baada ya Modi kuzungumza na kiongozi wa Russia Vladimir Putin, ambapo New Delhi ilisema Modi alieleza juu ya haja ya kuwepo mazungumzo na diplomasia ili kumaliza mgogoro huo.

Katika mkutano wa waandishi wa habari wa kawaida kufuatia wito wa Modi – Putin, Naibu msemaji mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Vedant Patel alisema akijibu suala kwamba “Nchi yoyote ambayo ina azma ya kujihusisha katika amani na inataka kumaliza vita hivi lazima ifanye hivyo kwa ushirikiano wa karibu na washirika wa Ukraine.”

India haijalaani moja kwa moja vitendo vya Russia kwa vita vyake kwa dhidi ya Ukraine na inaendelea kuwa na ushirikiano wa karibu na Moscow. Wakati wa ziara yake Moscow mwezi Novemba, waziri wa mambo ya nje wa India alisema India, ambayo imejitokeza kuwa mnunuzi mkubwa wa mafuta ghafi ya Russiaitaboresha ushirikiano wa kiuchumi na Moscow.

XS
SM
MD
LG