Russia ilianzisha mzozo huo kwa kumvamia jirani yake miezi 10 iliyopita, shirika la habari la Tass limemnukuu Lavrov akisema Ukraine “inaweza kusitisha ukaidi usiokuwa na maana wakati wote ule.”
Lavrov alisema Ukraine inayafahamu mapendekezo ya Russia kwa ajili ya “kuondoa majeshi na kusitisha siasa za kinazi” katika himaya ya Ukraine na kutokomeza vitisho vya Ukraine kwa Russia, ikiwemo maeneo manne ambayo Russia imeyachukua na kuyakalia.
Jumuiya ya kimataifa imerejea kupinga madai ya kuyakalia kimabavu maeneo hayo ikiwemo Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporizhzhia.
Lavrov aliongeza kuwa kama Ukraine haitayakubali madai ya Russia, “suala hilo litaamuliwa na jeshi la Russia.”
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema kuwa Russia inaweza kusitisha vita iliyoianzisha wakati wowote kwa kuondoa majeshi yake na kurejesha utawala wa Ukraine, uhuru na kuheshimu mipaka yake.
Baadhi ya taarifa hizi zinatokana na mashirika ya habari ya AP, Reuters and AFP.