Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 07:40

Mamia ya wakimbizi wa Myanmar wakimbilia India


Mamia ya wakimbizi wanakimbilia usalama nchini India, huku jeshi la Myanmar, likizidisha mashambulizi ya anga katika jimbo la kaskazini magharibi mwa Myanmar, Chin shirika la misaada ya wakimbizi liliiambia VOA Jumatano.

Takriban wakimbizi 200 wa Chin, walivuka mpaka wiki iliyopita kufuatia mashambulizi ya anga ya jeshi la Myanmar kwenye kambi muhimu ya waasi kwenye mpaka wa India na Myanmar, kulingana na Shirika la Haki za Kibinadamu la Chin (CHRO).

Shirika hilo, ambalo limeripoti takriban mashambulizi 14 ya anga baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Februari 2021, linafanya kazi kulinda na kukuza haki za watu wa Chin na jamii zingine zinazokandamizwa na kutengwa Myanmar.

XS
SM
MD
LG