Polisi wa India walivamia nyumba za waandishi kadhaa wa habari siku ya Jumamosi katika uchunguzi wa vitisho visivyojulikana mtandaoni kwa waandishi wa habari karibu darzeni moja huko Indian Kashmir, afisa wa ngazi ya juu wa polisi alisema.
Polisi wamelilaumu Laskhar-e-Toiba lenye makao yake nchini Pakistan na chama chake cha Resistance Front kwa vitisho hivyo. New Delhi imekuwa ikipambana na uasi wa wapiganaji wa Kiislamu wanaotaka kujitenga katika eneo linalozozaniwa la Himalaya tangu mwishoni mwa miaka ya 1980.
Mwandishi wa habari wa eneo hilo Sajad Ahmad Kralyari alikamatwa kwa mahojiano wakati wa uvamizi huo, na LAPTOP yake, kamera na simu za mkononi vilichukuliwa, afisa huyo aliliambia shirika la habari la Reuters kwa sharti la kutotajwa jina kwa sababu hakuwa na idhini ya kuzungumza na vyombo vya habari.
Uvamizi huo ulikuwa katika nyumba za waandishi wa habari nusu darzeni, akiwemo mwandishi wa vitabu Gouhar Geelani, afisa huyo alisema.
Geelani, Kralyari, na waandishi wengine hawakupatikana kuzungumzia suala hilo na simu zao zilizimwa.