Inspekta Jenerali Hillary Mutyambai Jumanne aliuambia mkutano wa maaskofu na viongozi wa juu wa dini kwamba wamegundua idadi ya kushangaza ya kesi baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu kwa maafisa wote wa polisi.
Kenya ina takriban maafisa laki moja wa polisi wanaofanya kazi katika jeshi hilo.
Bwana Mutyambai amesema walianza utaratibu wa kuwaondoa baadhi ya maafisa wa polisi walioathirika wakigusia umuhimu wa kuwa na polisi walio na akili timamu.
Hata hivyo amesema kuwaondoa maafisa hao katika kazi zao haikuwa rahisi kwa sababu ya mchakato unaohusika katika kuwaondoa.
Kumekuwa na wasiwasi zaidi katika miaka ya karibuni kuhusu akili za maafisa wa polisi na serikali ilianza kutatua suala hilo.
Bwana Mutyambai alisema kwa sasa polisi wana bodi ya kitaalamu ya afya inayojumuisha washauri na madaktari wa akili waliothibitishwa na Wizara ya Afya kutoa huduma ya afya ya akili.