Adhabu ya viboko ilipigwa marufuku katika shule za Kenya mwaka 2001 na sheria inawalinda watoto dhidi ya manyanyaso ya aina yoyote.
Lakini baadhi ya walimu wakuu wa shule za sekondari wanasema kuondolewa kwa adhabu kwa wanafunzi kunadumaza mamlaka ya waalimu.
Mwenyekiti wa muungano wa waalimu wa shule za sekondari nchini Kenya Kahi Indimuli, amesema kwamba kazi ya kusimamia nidhamu ya wanafunzi ni ngumu sana kwa shule yoyote.
Walimu wakuu wa shule za sekondari wanakutana wiki hii kwa kongamano la kila mwaka kujadiliana kuhusu visa vya utovu wa nidhamu vinavyoendelea kuongezeka nchini Kenya.
Shule kadhaa za sekondari nchini Kenya zilichomwa moto mwaka uliopita, wanafunzi wakitajwa katika visa hivyo.