Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:31

Kenya yawapa chakula wanyama pori kufuatia ukame


Mohamed Mohamud, askari wa wanyama pori kutoka Hifadhi ya Wanyamapori ya Sabuli, akiangalia mzoga wa twiga aliyekufa kutokana na njaa karibu na kijiji cha Matana, Kaunti ya Wajir, Kenya, Oct. 25, 2021.
Mohamed Mohamud, askari wa wanyama pori kutoka Hifadhi ya Wanyamapori ya Sabuli, akiangalia mzoga wa twiga aliyekufa kutokana na njaa karibu na kijiji cha Matana, Kaunti ya Wajir, Kenya, Oct. 25, 2021.

Shirika la Wanyamapori la Kenya limesema limelazimika kuingilia kati  ili   kuwaokoa  baadhi ya wanyama walioathiriwa na ukame wa muda mrefu katika maeneo ya hifadhi  na maeneo mengine nchini.

Shirika la KWS limesema limechimba visima na kupeleka mapipa ya maji baada ya vyanzo vya maji, ikiwemo mito ya vipindi kukauka.

Pia limetoa chakula kama vile nyasi katika baadhi ya hifadhi.

Madaktari wa wanyama wamekuwa wakizunguka katika hifadhi za wanyama kuwatambua walio wagonjwa na wenye afya duni ili kuwatibu pamoja na kufanya uchunguzi kuhusu wanyama waliokufa, KWS imesema.

Hata hivyo imeeleza kuwa mvua zilizonyesha nchini Kenya katika siku chache zilizopita zitasaidia kuleta afueni kwa wanyama wengi walioathiriwa na ukosefu wa maji na majani.

Kwa miezi kadhaa sasa, mamia ya wanyama pori wamekuwa wanakufa na wafugaji wameripoti hasara nyingi za mifugo yao kutokana na ukame mkali ambao umekumba mataifa yote ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika.

Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa WFP Jumanne limesema baadhi ya maeneo ya Ethiopia , Somalia na Kenya yamekabiliwa na kipindi cha ukame kwa miaka 40 iliyopita.

XS
SM
MD
LG