Mlipuko wa COVID-19 unaonekana umesababisha kuongezeka kwa msongo wa mawazo na wasiwasi ulimwenguni.
Kulingana na utafiti uliochapishwa katika jarida la afya la The Lancet, kulikuwa na mamilioni ya visa kama hivyo mwaka jana kuliko ilivyotarajiwa. Wanawake na vijana ndio waliokuwa miongoni mwa makundi yalioathirika zaidi na msongo wa mawazo unaohusiana na janga na wasiwasi.
Janga hili limeongeza limeongeza kwa haraka haja ya kuimarisha mifumo ya afya ya akili katika nchi nyingi, utafiti huo ulisema. Kutochukua hatua yoyote ya kushughulikia mzigo wa shida kubwa ya msongo wa mawazo na matatizo ya wasiwasi haipaswi kuwa jambo la kuchagua,watafiti walisema.
Siku ya Ijumaa, wizara ya afya ya Brazil ilisema idadi ya vifo vya COVID-19 katika nchi hiyo imevuka 600,000. Kituo cha Rasilimali cha Johns Hopkins kinachofuatlia virusi vya corona kimerekodi visa milioni 21.5 vya COVID-19 katika nchi za Amerika Kusini.