Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:06

Marekani yatenga dola milioni 5 kwa ajili ya Haiti


Silaha zilizopatikana na maafisa wa usalama kutoka kwa wahalifu nchini Haiti. Ukosefu wa usalama umeongezeka nchini humo
Silaha zilizopatikana na maafisa wa usalama kutoka kwa wahalifu nchini Haiti. Ukosefu wa usalama umeongezeka nchini humo

Marekani imetangaza kutenga dola milioni 5 kutoka katika Mfuko wake Mkuu wa Majibu ya Dharura (CERF), illi kushughulilkia hali mbaya inayoongozeka iliyosababishwa ghasia za magenge.

Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yanasema kwamba tangu mwezi Julai, takriban watu 500 wameuawa katika mapambano kati ya magenge huko Cite Soleil nchini Haiti, eneo maskini sana na lenye idadi kubwa ya watu katika mji mkuu, Port au Prince.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu inakadiria kwamba takriba watu 280,000 wamekwama katika mapigano. Idara hiyo inaonya kuwa hali inazidi kuwa mbaya sana huku ghasia zikiongezeka na kuwanyima watu chakula, maji ya kukunywa na huduma za afya.

Msemaji wa OCHA Jens Laerke anasema fedha zimetolewa na CERF kuyasaidia masharika ya kibinadamu ambayo hayana fedha za kutosha ili kujibu mahitaji ya haraka ya wahaiti. Amekiri kwamba dola milioni 5 ni kiwango kidogo lakini anasema ni kiasi cha fedha muhimu sana hivi sasa.

“Ufadhili kupitia UNICEF na WFP, wenzetu watatoa chakula, majir ya kunywa, huduma za afya, afya ya akili na elimu kuwasaidia zaidi ya watu 100,00 kwa jumla…. Kinachotoka mara kwa mara tunapotoa pesa kutoka CERF ni kwamba wafadhili wengine nao wanafuatia, kwa kweli, kwa ujumbe na ishara kwamba hili ni muhimu sana katika kuokoa maisha na kuingilia kati kunahitajika hivi sasa.”

UNICEF inasema kiasi cha 20% ya watoto huko Cite Soleil walio na umri wa chini ya miaka mitano wataabishwa na utapiamlo wa kawaida au uliokithiri. Inasema maelfu wako katika hatari ya kufa kwasababu ya ghasia za magenge ambazo zinawazuia kupata huduma zinazostahili za afya na lishe.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani linasema karibu nusu ya idadi ya watu nchini Haitik kiasi cha milioni 4.4 wana shida ya chakula. Laerke anasema kuwapatia misaada watu wengi wenye shida kuna changamoto.

XS
SM
MD
LG