Katika michezo ya Olimpiki Tokyo, suala la afya ya akili lilikuwa linaongoza kujadiliwa. Likipaziwa sauti na baadhi ya wanariadha wa juu duniani, lilitikisa Michezo hiyo na kumfanya kila mtu atambue hilo.
Miezi sita baadae, mjini Beijing, mazungumzo yamejirudia: Suala hilo linajitokeza mara kwa mara, lakini hakuna aliyeshangazwa lilipojitokeza.
Wanariadha wengi wamezungumza jinsi wanavyohangaika, lakini aghlabu ilikuwa usilikuze, hakuna cha kuchunguzwa.
Ugumu unatajwa, na kisha mazungumzo yanaendelea. Baada ya nyota wa mazoezi ya viungo Simone Biles alipojitoa katika mashindano ya Tokyo kwa sababu hakuwa katika hali nzuri, muogeleaji wa Olimpiki aliyestaafu Michael Phelps ikikumbukwa alisema kuwa “Ni sawa kutokujisikia vizuri.”
Na hivi leo, tunashukuru kwa upande mmoja kwa watu kama Biles, inaonekana ni sawa kuzungumzia hali hiyo.
“Nafikiri funzo kubwa zaidi nililojifunza baada ya Olimpiki ya mwisho kuwa muwazi kadri inavyowezekana,” nyota wa mashindano ya kuteleza katika theluji Chloe Kim aliwaambia waandishi wa habari baada ya kunyakuwa medali ya dhahabu Alhamisi baada ya mashindano.
Ilikuwa medali ya pili ya dhahabu aliyoshinda Kim. Mwanzoni aliitupa ya kwanza katika jalala aliyoshinda Pyeongchang miaka minne iliyopita – ni habari inayobaini sura ya furaha ya nyota wengi wa michezo wanauonyesha ulimwengu na maumivu wanayokabiliana nayo kwa siri.
“Baada ya Olimpiki ya mwisho, nilijiwekea shinikizo mimi mwenyewe ili niwe sawa wakati wote, na hilo lingesababisha masuala mengi nyumbani. Kwa kweli nilikuwa mwenye huzuni na msongo wa mawazo wakati wote nilipokuwa nyumbani,” Kim aliwaambia waandishi wa habari baada ya kufikia nafasi ya juu katika jukwaa – lakini pia kushindwa kufikia mbinu mpya aliyokuwa anaifanyia mazoezi.
“Ninafuraha kuzungumzia chochote kile nilichokuwa napitia,” alisema. “Ukweli, ni kitu chenye afya kwangu.”
Siyo tu Kim anayezungumzia hilo. Baada ya nyota wa kuteleza katika theluji Jamie Anderson, aliyekwenda Beijing kama mtetezi wa ushindi wa mashindano ya kwenye mteremeko, alimaliza wa tisa, aliweka katika mtandao wa Instagram kuwa “afya ya akili na utulivu havijafikiwa.
Nyota wa mashindano ya theluji Mikaela Shiffrin alikuwa hasa mkweli baada ya kushindwa kukamilisha mbio zote mbili za kwanza katika matukio ambayo yeye amejikita nayo. Alisema kuwa alikuwa anahisi shinikizo, kitu ambacho kila mwanariadha mahiri anakihisi na kinajitokeza kuwa ni hali ngumu zaidi katika changamoto za afya ya akili ambapo wengi wamekuwa wakizungumzia.
Lakini Shiffrin alienda mbali zaidi, kukiri kuwa alikuwa amemkasirikia baba yake, aliyekufa mwaka 2020, kwa kutokuwepo naye kumuunga mkono katika mashindano hayo.