Taasisi ya Sweden ya Tafiti za Kisayansi imetangaza Jumatatu imetoa tuzo hizo kwa Abhijit Banerjee, Mmarekani aliyezaliwa India, Mfaransa – Mmarekani Esther Duflo, na Mmarekani Michael Kremer.
Duflo ni mwanamke wa pili kupata tuzo kwenye fani ya uchumi katika historia.
Taasisi hiyo imesema wachumi hao walianzisha utaratibu mpya wa kuleta njia bora za kupambana na umaskini, wakiangaza masuala madogo kama vile jinsi ya kuboresha afya na elimu ya mtoto.
Washindi hao watagawana tuzo hiyo ya dola 915,300.