Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:09

Waziri Mkuu wa Ethiopia ashinda tuzo ya Amani ya Nobel 2019


Waziri Mkuu Abiy Ahmed Ali
Waziri Mkuu Abiy Ahmed Ali

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed Ali, ameshinda tuzo ya Amani ya Nobel 2019 kwa juhudi zake za kutafuta Amani na jirani zake Eritrea.

Mwenyekiti wa kamati yenye wajumbe watano wanaoteuwa tuzo ya Nobel, Berit Reiss Andersen alisema tuzo hiyo ya Amani ambayo Abiy aliteuliwa kuipata inatokana na juhudi zake mbadala za kumaliza mgogoro wa nchi yake na Eritrea ndani ya kipindi cha miezi kadhaa tangu aingie madarakani mwaka 2018.

Kamati hiyo inakiri kwamba kazi kubwa bado inahitajika kufanywa kuimarisha demokrasia nchini Ethiopia, lakini matumaini ya mkataba wa Amani na Eritrea yataongoza kuwepo mabadiliko yenye matumaini kwa nchi zote hizo mbili.

Kamati ya tuzo ya Amani ya Nobel pia ilimtambua Abiy kwa kujishughulisha kwake katika kuleta Amani na mashauriano kwenye maeneo mengine huko mashariki na kaskazini mashariki ya Afrika. Tuzo ya kiasi cha dola laki tisa itakabidhiwa kwake mjini oslo hapo Dsemba 10.

Tuzo ya Amani katika sayansi ya kiuchumi itatolewa Jumatatu Oktoba 14.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG