Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:48

Ethiopia: Maelfu wamiminika Addis kwa sikukuu ya 'Ireecha'


Maelfu ya wanawake wajiunga na wanaume na watoto kusherehekea sikukuu ya "Ireecha" mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Maelfu ya wanawake wajiunga na wanaume na watoto kusherehekea sikukuu ya "Ireecha" mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Maelfu ya watu wa jamii ya Oromo, Jumamosi walikusanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, kuadhimisha sikukuu ya kila mwaka iitwayo Ireecha, ambayo huashiria kumalizika kwa msimu wa mvua na kuanza kwa kipindi cha mavuno.

Tangu Alhamisi, usalama ulikuwa umeimarishwa kwenye barabara mbalimbali za mji huo.

Kuanzia Ijumaa, maelfu wa watu waliendelea kuwasili mjini Addis Ababa kutoka maeneo mbalimbali wakiwa wamejivika mavazi ya kitamaduni huku wakiimba nyimbo, kucheza densi na kupeperusha vijibendera.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba sherehe hizo ziliendelea bila vuruguu yoyote licha ya hali ya taharuki kutanda katika baadhi ya sehemu za mji huo.

Kwa muda sasa, viongozi wakuu wa kabila la Oromo kwamekuwa wakidai kwamba wanamiliki mji wa Addis Ababa kwa sababu "uko katika eneo letu la Oromoia."

Kwa kawaida kauli za viongozi hao, hazipokelewi vyema na jamii zingine ambazo zinamiliki ardhi na majengo ya biashara kwenye mji huo mkuu.

Sherehe za "Ireecha"
Sherehe za "Ireecha"

Kwa kawaida, sherehe hizo hufanyika katika mji wa Bishofu kwenye eneo la Oromia, lililo takrinban kilomita 50 Kusini Mashariki mwa Addis Ababa.

Maadhimisho kama hayo ya mwaka wa 2016 yalikumbwa na ghasia na vurugu na kupelekea vifo vya Zaidi ya watu 50.

XS
SM
MD
LG