Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, hatua hiyo ni katika juhudi za kuimarisha taswira ya kampuni hiyo ambayo hadhi yake imeshuka kwa kiwango kikubwa katika siku za karibuni,
Hii ni kufuatia ajali ya mwezi Machi mwaka huu iliyozua utata, ambapo abiria wote 157 wa ndege ya shirika la Ethiopia Airlines waliokuwa safarini kutoka Addis Ababa, Ethiopia, kwelekea Nairobi Kenya na ile ya ndege ya shirika la Indonesia Airlines iliyotokea mwaka wa 2018.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Dennis Mullenburgh, alisema kupitia taarifa, kwamba pesa hizo zitatolewa kwa kipindi cha miaka kadhaa ijayo.
Hata hivyo, hakutoa mfedha hizo, wala utaratibu utakaofuatwa.
Boeing inaendelea kuchunguzwa na taasisi mbalimbali na inakabiliwa na takriban kesi 100 zilizowasilishwa na familia za waathiriwa wa ajali hizo mbili.
Kwa jumla, watu 346 walipoteza maisha yao kwenye ajali hizo mbili.