Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:14

Daktari Mukwege wa DRC ashinda tuzo ya Nobel 2018


Dkt Denis Mukwege akiwa na wagonjwa katika hospitali ya Panzi, Bukavu, Mashariki ya DRC.
Dkt Denis Mukwege akiwa na wagonjwa katika hospitali ya Panzi, Bukavu, Mashariki ya DRC.

Tuzo ya Nobel 2018 imetolewa kwa Mtaalam wa magonjwa ya wanawake nchini Kongo, Denis Mukwege, kutokana na kazi yake ya kuwatibu waathiriwa wa ukatili wa kingono katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mukwege ameshinda tuzo hiyo pamoja na Nadia Murad, mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka kabila la Yazidi na manusura wa utumwa wa kingono unafanywa na kikundi cha Islamic State Iraq.

Tuzo ya amani inatolewa pamoja na Dola za Marekani milioni 1.1.

Kamati ya tuzo ya Nobel yenye makao yake Norway, imesema kwamba imetoa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wao katika kumaliza matumizi ya ukatili wa kingono kama silaha ya vita na migogoro ya kivita.

Mukwege, 63, anaendesha hospitali ya Panzi iliyoko mashariki mwa DRC,eneo lenye vita ambako makundi yenye silaha yametumia uhalifu wa kingono kuwaweka katika vitisho wananchi wa sehemu hiyo. Bukavu, mji mkuu wa Kivu kusini, ambapo hospitali hii imekuwa ikitoa tiba kwa mamia ya wanawake wanao najisiwa kila mwaka.

Idadi ya wanawake wanaonajisiwa kila mwaka nchi Congo haijulikani, lakini wataalam wanasema kwamba ni kubwa.

Aliyekuwa mwakilishi wa umoja wa mataifa kuhusu dhuluma za ngono Margot Wallstrom, ametaja Congo kuwa jiji kuu la dunia kwa unajisi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema Ijumaa kuwa Mukwege amekuwa ni shujaa kwa kulinda haki za wanawake ambao wamejikuta katikati ya vita na kudhalilishwa kingono, kunyanyaswa na aina nyingine za unyanyasaji.

Tuzo ya Nobel kwa ajili ya tiba, fizikia na kemia zilitolewa mapema wiki hii. Tuzo ya fasihi haikutolewa mwaka huu kwa sababu ya kashfa ya ngono iliyo gubika chombo kinacho toa tuzo hiyo.

Tuzo ya kumbukumbu ya Nobel ya sayansi ya uchumi itatolewa Jumatatu, Octoba 8.



XS
SM
MD
LG