Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:05

Wamarekani wapokea tuzo ya Nobel ya uchumi


William Nordhaus wa Chuo Kikuu cha Yale na Paul Romer wa Chuo Kikuu cha New York
William Nordhaus wa Chuo Kikuu cha Yale na Paul Romer wa Chuo Kikuu cha New York

Watafiti wawili wa Marekani wameshinda tuzo ya Nobel ya 2018 ya uchumi.

William Nordhaus wa Chuo Kikuu cha Yale na Paul Romer wa Chuo Kikuu cha New York watashirikiana katika tuzo hiyo ya Dola za Marekani milioni 1.01.

Tamko lililotolewa na Taasisi ya Elimu ya Royal Swedish of Sciences limesema, “Washindi wa mwaka huu… kwa umuhimu mkubwa wameweza kupanuwa wigo wa uchambuzi kwa kutengeneza vigezo mbalimbali vinavyo elezea jinsi gani masoko ya kiuchumi yanavyo kabiliana na tabia na ujuzi.

Hivi karibuni tuzo ya Nobel 2018 ilitolewa kwa mtaalam wa magonjwa ya wanawake nchini Kongo, Denis Mukwege, kutokana na kazi yake ya kuwatibu waathiriwa wa ukatili wa kingono katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mukwege ameshinda tuzo hiyo pamoja na Nadia Murad, mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka kabila la Yazidi na manusura wa utumwa wa kingono unafanywa na kikundi cha Islamic State Iraq.

Tuzo ya amani inatolewa pamoja na Dola za Marekani milioni 1.1.

XS
SM
MD
LG