Kwa mshangao kamati ya tuzo ya Nobel ilitangazsa Ijumaa kwamba tuzo yake ya amani kwa mwaka 2016 inapewa rais wa Columbia, Juan Manuel Santos, kwa juhudi zake za kufikia makubaliano ya amani na kundi la waasi la Revolutionary Armed Forces of Colombia FARC, na hivyo kumaliza mapigano ya muda mrefu kabisa katika mabara ya Amerika.
Hatua hiyo inachukuliwa kua ni mshangao kutokana na kwamba siku ya Jumapili wapiga kura wa Colombia walipinga makubaliano hayo kwa wingi mdogo.
Akitangaza tuzo hiyo ya Amani mwenyekiti wa kamati ya Nobel, Kaci Kullman, Five alisema kupingwa kwa makubaliano hayo hayapunguzi mafanikio ya rais Santos.
Amesema wapiga kura hawajapinga haja ya kuwepo na Amani lakini walipinga mkataba huo wa Amani. Kamati imezihimiza pande zote kuendelea na mjadala wa kitaifa kuendelea na utaratibu wa Amani.
Kiongozi wa FARC, Timoleon Jimenez, ambaye pia anajulikana kama Timochenko, mwezi uliopita alitia saini mkataba wa kumaliza mapigano na Rais Santos.