Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:04

Kazuo Ishighuro apata tuzo ya fasihi ya Nobel


Mashabiki wa mshindi wa Nobel Prize wakisherehekea tuzo ya Kazuo Ishighuro huko Tokyo, Japan, October 5, 2017.
Mashabiki wa mshindi wa Nobel Prize wakisherehekea tuzo ya Kazuo Ishighuro huko Tokyo, Japan, October 5, 2017.

Tuzo ya fasihi ya Nobel inayotolewa na Taasisi ya Taaluma ya Uswidi kuhusu Lugha na Fasihi imenyakuliwa na raia wa Uingereza Kazuo Ishighuro mwenye umri wa miaka 62.

Kazuo Ishighuro aliyetunukiwa tuzo katika hali ambayo wengi wanaeleza kuwa ya kushtukiza, alihamia Uingereza kutoka Japan akiwa na umri wa miaka mitano.

Kazi yake ya Fasihi iliompa umaarufu mwingi ni ‘Remains of the Day’ ‘Let me Go’ na ‘The Buried Giant’, vitabu alivyoviandika kwa Lugha ya Kiingereza.

Mshindi wa tuzo hii hupokezwa kitita cha fedha ambacho ni takribani $1,110,000 pamoja na kifurushi cha dhahabu Desemba 10 kila mwaka. Tuzo hizi zilianzishwa na Alfred Nobel ambaye alikuwa Mwanasayansi kutoka Uswidi aliyefariki mwaka 1986.

Watunzi wa vitabu waliokuwa wamepigiwa upatu kupata tuzo hii ni Mwandishi na Mhariri mwenye usuli wa Italiano Claudio Magris, Mhispania Javier Marias, Mjapani Haruki Murakami na Margaret Atwood kutoka Canada.

Wengine waliowahi kutunukiwa tuzo hii kutoka Afrika ni Albert Camus wa Algeria (1957), Wole Soyinka wa Nigeria (1986), Naguib Mahfouz wa Misri (1988), Nadine Gordimer wa Afrika Kusini (Afrika Kusini), John Maxwell Coetzee wa Afrika Kusini (2003), Doris Lessing (2007).

Wachambuzi wa masuala ya fasihi wanasema kuwa Prof. Ngugi Wa Thiong’o tangu mwaka wa 2010 amekuwa akipigiwa upatu kushinda tuzo hii lakini bado hajabahatika.

Profesa Ngugi mwenye umri wa miaka 79 aliandika kitabu chake cha kwanza kwa lugha ya kiingereza mwaka 1964. Miongoni mwa vitabu alivyoviandika ni ‘Weep Not Child’, ‘A Grain of Wheat’, ‘The River Between’ miongoni mwa vingine alivyoviandika kupitia lugha yake ya kiasili.

Prof. Walibora ambaye ameandika vitabu kadha wa kadha vikiwemo riwaya ya ‘Siku Njema’, ‘Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine’, ‘Kidagaa Kimemwozea’, ‘Pepela na Mto’ miongoni mwa vingine, anasisitiza kuwa hatua hii haimtoi matumaini Prof. Ngugi Wa Thiong’o kwani ni hali aliyoizoea.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:39 0:00

Imetayarishwa na mwandishi wetu Kennedy Wandera, Kenya

XS
SM
MD
LG