Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 23:54

Wapiganaji wa Islamic State waukimbia mji wa Hawija


Vikosi vya pamoja vya Iraq vikiwa katika hatua za mwisho kuuteka mji wa Hawija
Vikosi vya pamoja vya Iraq vikiwa katika hatua za mwisho kuuteka mji wa Hawija

Vikosi vya pamoja vya Iraq vimeuteka mji wa Hawija kutoka katika himaya ya kikundi cha wapiganaji wa Islamic State, Waziri Mkuu wa nchi hiyo amesema Alhamisi.

Haider al-Abadi ametangaza ushindi huo katika mkutano wa waandishi wa habari akiwa na Kiongozi wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Paris, akiuita kuwa “sio ushindi wa Iraqi peke yake, lakini wa ulimwengu mzima.”

Vikosi vya Iraq vinavyoungwa mkono na Marekani vikishirikiana na vya washia vinavyoungwa mkono na Iran vimefanya operesheni hiyo katika mji wa Hawija, ambayo ilianza septemba 21.

Luteni Jenerali Paul Funk msimamizi mkuu wa vikosi vya pamoja vinavyofanya operesheni huko Iraq vimepongeza wapiganaji wa Iraq kwa kuuteka mji huo “ walipigana kwa ujasiri na kwa weledi mkubwa dhidi ya adui muovu na aliyejiandaa.”

Kwa mujibu wa taarifa ya kikosi kazi cha jeshi la pamoja mapigano hayo yamechukuwa siku 14 na zaidi ya magaidi 1,000 wamejisalimisha.

Mji huo ulioko kaskazini mwa Iraq umekuwa ngome ya Islamic State lakini kundi hilo lingali linashikilia baadhi ya sehemu karibu na mpaka wa Syria. Kundi hilo pia linashikilia baadhi ya miji kwenye jimbo la magharibi la Anbar.

Vikosi vya Iraq vimechukua tena karibu kila sehemu ilioshikiliwa na Islamic State ukiwemo mji wa Mosul ulio wa pili kwa ukubwa nchini humo.

XS
SM
MD
LG