Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 07:06

Salman ni Mfalme wa Saudia wa kwanza kuzuru Moscow


Mfalme Salman (C) na Naibu Waziri Mkuu wa Russia, Dmitry Rogozin (R).
Mfalme Salman (C) na Naibu Waziri Mkuu wa Russia, Dmitry Rogozin (R).

Mfalme Salman wa Saudi Arabia yuko Moscow katika ziara yake ya kwanza kuwahi kufanywa na mfalme yoyote wa Saudi Arabia nchini Russia.

Katika ziara ya siku nne mfalme anatarajiwa kukutana na Rais wa Russia Vladimir Putin kwa mazungumzo kuhusu masuala mbali mbali kuanzia mafuta mpaka Syria.

Ziara yake inaashiria kuimarika kwa uhusiano kati ya mahasimu hao wawili wa kihistoria na kusukuma haja ya kushughulikia kushuka kwa bei ya mafuta ulimwenguni.

Mfalme Salman (C) na Naibu Waziri Mkuu wa Russia, Dmitry Rogozin. Oct. 4, 2017.
Mfalme Salman (C) na Naibu Waziri Mkuu wa Russia, Dmitry Rogozin. Oct. 4, 2017.

Uhasimu kati ya wazalishaji wawili wakubwa wa mafuta duniani unarejea wakati wa enzi za vita baridi ambapo Saudi Arabia ilikuwa inawasaidia waasi wa Afghanistan dhidi ya uvamizi wa Soviet.

Katika siku za karibuni mivutano imekuwa juu kutokana na vita nchini Syria ambapo Russia inaiunga mkono serikali ya Rais Bashar al-Assad wakati Saudi Arabia inawaunga mkono waasi wanaojaribu kuiangusha serikali ya Assad.

XS
SM
MD
LG