Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:28

Wanasheria waishtaki serikali ya Trump ili kuwanusuru watoto wahamiaji


FILE - Watoto wahamiaji wakipanga mstari kuingia katika makazi ya muda (Mahema) Aprili 19, 2019. Mawakili wanasema mazingira ya makazi haya ni sawa na jela.
FILE - Watoto wahamiaji wakipanga mstari kuingia katika makazi ya muda (Mahema) Aprili 19, 2019. Mawakili wanasema mazingira ya makazi haya ni sawa na jela.

Makundi mbalimbali ya wanasheria wamefungua mashtaka dhidi ya serikali ya Marekani Ijumaa kujaribu kuzuia kuondolewa nchini watoto waliokuwa wamefungiwa katika vyumba vya hoteli na uongozi wa Trump chini ya tamko la dharura likieleza ni kutokana na virusi vya corona.

Wamiliki wa Hoteli ya Hampton Inn & Suites huko McAllen, Texas, wamesema Ijumaa usiku kuwa wamesitisha kupokea maombi ya wateja wapya kuingia katika vyumba hivyo ambavyo watoto walikuwa wamefungiwa ndani, limeripoti shirika la Habari la AP.

Vyombo vya Uhamiaji na Forodha vimethibitisha kuwa watoto wote wameshaondolewa hotelini, siku mbili baada ya shirika la Habari la Associated Press kuripoti kuwa hoteli hiyo ni kati ya hoteli tatu zilizotumika zaidi ya mara 200 kuwashikilia watoto ambao wengine ni chini ya umri wa mwaka mmoja.

Lakini ICE mara kadhaa imekataa kujibu maswali yanayohusu wakandarasi wapi wamewapeleka watoto hao, wakieleza hatari kwa usalama wao.

“Uongozi wa Trump unawashikilia watoto katika hoteli kwa siri, ukikataa kuwaruhusu mawakili kuwasiliana watoto hao ili ICE iwaondoe kwa nguvu nchini kuwarudisha katika hatari bila ya kuwapa fursa watoto hao kuonyesha ushahidi wa kuwa wanastahili kupewa hifadhi nchini,” amesema Lee Gelernt, Wakili wa Jumuiya ya American Civil Liberties, iliyofungua kesi kwa niaba ya Mradi wa Haki za Kiraia Texas.

Gelernt amesema kufungua mashtaka kwa niaba ya watoto wasiotajwa majina yao ni muhimu “kwa sababu serikali inakataa kutoa maelezo juu ya watoto hao.”

Mashtaka hayo yamefunguliwa katika Mahakama ya serikali kuu Washington, na Gelernt amesema ataomba kuingiza majina ya mtoto yoyote aliyeshikiliwa katika hoteli hadi kufikia Alhamisi.

Takwimu za serikali zilizokusanywa na Shirika la Habari la AP zinaonyesha watoto walishikiliwa mara 123 katika Hoteli ya McAllen mwezi Aprili na Juni.

Castle Hospitality, ambayo inaiendesha McAllen ilikataa kusema ni vyumba vingapi vilikuwa vimetumika na ICE au wakandarasi binafsi, MVM Inc.

Hoteli nyingine za Hampton Inns ziko karibu na viwanja vya ndege huko Phoenix na El Paso, Texas, kwa mujibu wa takwimu walizopata AP.

Chini ya sheria ya serikali kuu ya kuzuia biashara ya binadamu na makubaliano ya mahakama, watoto wengi wanaovuka kuingia Marekani kutokea mpaka wa Mexico wanatakiwa kuwekwa katika nyumba vinavyoendeshwa na Wizara ya Afya na Huduma za Binadamu na hatimaye kukabidhiwa kwa familia ambazo huwadhamini.

Lakini utawala wa Trump unasema ni lazima wawaondoe nchini watoto ili kuzuia kuenea COVID-19, ukinukuu tamko la dharura lilitolewa mwezi Machi na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani.

Watoto wasiopungua 2,000 tangu wakati huo wameondolewa kwa nguvu Marekani bila ya kupewa fursa ya kuomba hifadhi.

XS
SM
MD
LG