Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:20

Trump apendekeza sera za uhamiaji ikiwa ni sharti la kufungua serikali


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Katika jitihada za kumaliza sakata la kufungwa kwa baadhi ya idara za serikali Marekani kwa kipindi cha mwezi mmoja, Rais DonaldTrump Jumamosi alitoa pendekezo la kufikia makubaliano na Wademokrat juu ya sera zake za uhamiaji zenye msimamo mkali, lakini zimetupiliwa mbali na chama cha upinzani hata kabla yakuongea.

“Ni matumaini yetu kuwa watatuunga mkono kwa nia ya dhati, na nafikiri wengi watafanya hivyo,” Trump alisema hilo juu ya Wademokrat. “Mrengo wa kushoto wenye msimamo mkali hauwezi kudhibiti mipaka yetu. Sitaruhusu hilo kutokea.”

Katika maelezo yake yaliyo rushwa hewani mubashara kutoka White House, Trump ametaka waajiriwe wafanyakazi zaidi 2,750 wa serikali kuu watakao dhibiti wahamiaji haramu mipakani na dola za Marekani bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa chuma wenye urefu wa kilomita 370 (maili 230) katika mpaka wa Marekani na Mexico.

Spika wa baraza la wawakilishi Nancy Pelosi, amesema pendekezo la RaisTrump ni mkusanyiko wa mikakati yake kadhaa ya awali ambayo ilikataliwa na isiyokubalika.

Trump pia alitoa pendekezo la kufikia makubaliano ili serikali ifunguliwe, akizungumzia hatma ya vijana walioingia nchini humo kinyume cha sheria wakiwa watoto, sharti ni kuwa Wademokrat waidhinisha fedha za kugharamia ujenzi wa ukuta.

Trump alitoa pendekezo la kufikia makubaliano kwa programu mbili ambazo uongozi wake unataka kuzifuta: kucheleweshwa kuchukuliwa hatua kwa vijana walioingia nchini wakiwa watoto (DACA) na hadhi ya hifadhi ya muda kwa wahamiaji kutoka Amerika ya Kati na nchi za Kiafrika

Sheria ya ushirikiano baina ya vyama hivyo inayo julikana kama Bridge Act itawawezesha wahamiaji 740,000 ambao waliingia Marekani kinyume cha sheria wakiwa Watoto, ambao ni maarufu kama Dreamers, kuendelea kutumia vibali vya kufanya kazi na kuzuia kuondoshwa nchini kwa miaka mitatu zaidi kama tayari vibali vyao vimefutwa. Lakini baadhi ya Waconservative maarufu wanaochangia maoni yao wamepinga vikali mpango huu.

XS
SM
MD
LG