Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:57

Baraza la seneti Marekani limepiga kura kuanza mjadala wa DACA


Seneta Cory Booker, mdemocrat akizungumza juu ya suala la DACA
Seneta Cory Booker, mdemocrat akizungumza juu ya suala la DACA

Baraza la seneti la Marekani lilipiga kura 97 dhidi ya 1 Jumatatu jioni ili kuanza majadiliano ya kina juu ya mageuzi ya uhamiaji huku tofauti kati ya vyama zikijitokeza haraka juu ya malengo na kutoa mwangaza katika kile wabunge wanachotumaini kuona katika hatua za mwisho za mjadala huo.

Kiongozi wa walio wengi katika baraza la senet m-Republican, Mitch McConnell
Kiongozi wa walio wengi katika baraza la senet m-Republican, Mitch McConnell

Kiongozi wa walio wengi katika baraza la seneti Mitch McConnell, m-Republican kutoka jimbo la Kentucky kwa maneno yake alisema “ninamatumaini baraza hili litaweza kuchukua fursa hii na kuleta maendeleo ya kweli”.

Mjadala huru wa siku kadhaa unatarajiwa kushika kasi wakati tarehe ya mwisho inakaribia kwa maelfu ya vijana wahamiaji ambao waliletwa nchini Marekani na wazazi wao wakati wakiwa watoto. Mwaka jana Rais Donald trump alisitisha mpango wa DACA ambao uliwalinda kwa muda wahamiaji vijana kuweza kufukuzwa Marekani na kulipa bunge muda hadi Machi tano mwaka huu kuandaa mswaada unaoelezea nafasi ya vijana hao ya ukaazi halali.

XS
SM
MD
LG