Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:13

Trump aepusha serikali kufungwa kwa kupitisha dola trilioni 1.3


Rais Donald Trump akielezea muswada wa dola trilioni 1.3
Rais Donald Trump akielezea muswada wa dola trilioni 1.3

Rais Donald Trump amepitisha muswada wa matumizi ya dola za Kimarekani trilioni 1.3 Ijumaa kwa shigo upande, masaa kadhaa baada ya kutishia kuzuia hatua hiyo kwa sababu ilikuwa haiwatetei wahamiaji waliokuja Marekani wakiwa watoto wadogo na wala kutenga fedha za ujenzi wa ukuta mpakani.

Katika shughuli hiyo ya haraka iliyoandaliwa na Ikulu ya Marekani Ijumaa mchana, Trump aliwaambia kikundi cha waandishi wa habari kuwa alisaini fungu hilo kubwa la fedha “ kwa sababu za usalama wa taifa” japokuwa alikuwa “hajaridhishwa na vitu vingi sana” katika fungu hilo kubwa la fedha lililotengwa.

“Kamwe sitasaini muswada mwengine kama huu. Sitofanya jambo hili tena,” amesema. “Hakuna mtu aliyesoma muswada huu. Una saa chache tangia uletwe. Baadhi ya watu hata hawajui – dola trilioni 1.3, ni fungu kubwa la pili kuliko yote.”

Kusaini kwake kwa muswada huo kumeepusha serikali kuu kufungwa saa sita usiku Ijumaa.

Trump amewaambia kikundi cha waandishi alikuwa alikuwa “ametafakari sana kuzuia muswada huo” lakini akaamua kusaini kutokana “na manufaa yasiyokadirika” kwa jeshi la Marekani.

Hatua hiyo amesema itafanya jeshi liweze kujikimu na kutoa ongezo kubwa la malipo kwa wanajeshi wa Marekani kwa zaidi ya muongo mmoja.

Pia itaongeza matumizi ya ulinzi kwa zaidi ya dola bilioni 60 kutoka mwaka 2017. Ikiwa ni sehemu ya muswada huo, jumla ya matumizi ya ulinzi yataongezeka kufikia dola bilioni 700, ongezeko kubwa kuliko yote katika kipindi cha miaka 15.

Katika tukio hilo la kusaini muswada ambalo lilirushwa moja kwa moja na televisheni kutoka Chumba cha Diplomasia cha Ikulu ya Marekani, Rais anayetokana na chama cha Republikan aliwalaumu wa Demokrat kwa kushindwa kuwatetea vijana wa DACA walioingizwa Marekani na wazazi wao wakiwa watoto wadogo kwa kuingiza suala lao katika muswada huo.

“Wanufaika wa DACA wametendewa vibaya sana na Wademokrati. Tulitaka kuwaingiza katika muswada huu, watu 800,000 na pengine ni zaidi ya hao. Tulitaka kuwaingiza katika muswada huu. Wademokrati hawawezi kufanya hili,” Rais alisema.

Wanufaika wa DACA ni wahamiaji wasiosajiliwa walioletwa nchini Marekani wakiwa watoto. Walikuwa wamelindwa na programu ya DACA iliyokuwa imesimamisha kwa muda hatua ya kuwaondosha nchini watoto hao wanapowasili, iliokuwa imeanzishwa mwaka 2012.

Trump hata hivyo aliisitisha programu hiyo mwisho wa mwaka jana wakati akilipa bunge la Marekani miezi sita kuandaa mpango wa kudumu kwa wanufaika wa DACA.

Pamoja na juhudi yote iliyofanywa na Wademokrati, muswada huo haukutaja kabisa suala la kuwalinda watoto hao wenye ndoto ya maisha bora. Wademokrati walikuwa wametoa wito kwa viongozi wa Republikan kuleta mapendekezo mbalimbali kwenye Ukumbi wa Bunge kutafuta suluhu juu ya suala la DACA.

Wakati huohuo, majaji wa serikali kuu wametoa agizo kwa uongozi wa Trump kuendelea kuziacha baadhi ya vifungu vya programu ya DACA wakati changamoto mbalimbali za kisheria zikijadiliwa katika mifumo ya mahakama.

XS
SM
MD
LG