Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:19

Suala la DACA bado ni kigugumizi bungeni Marekani


Waandamanaji wakiutetea mpango wa DACA, Jan. 3, 2018.
Waandamanaji wakiutetea mpango wa DACA, Jan. 3, 2018.

Huku zikiwa zimebaki takribani siku mbili kabla ya bajeti ya serikali kuu ya Marekani kuisha uwezekano wa kufikiwa makubaliano juu ya suala la uhamiaji liliendelea kuwa kizungumkuti hadi Jumatatu jioni ambapo Rais Donald Trump anakataa vielelezo muhimu vya pendekezo la vyama vyote vilivyowasilishwa katika baraza la seneti.

Rais Trump akiwa Blue Ash, Ohio. Feb. 5, 2018.
Rais Trump akiwa Blue Ash, Ohio. Feb. 5, 2018.

Rais Trump aliandika kwenye Twitter kwamba “makubaliano yeyote juu ya DACA ambayo hayajumuishi usalama thabiti wa mpaka na ujenzi wa ukuta ni kupoteza muda” akirudia tena baadhi ya madai yake ya kuidhinisha njia kutoa uraia kwa maelfu ya vijana wahamiaji wasiokuwa na hati halali za ukaazi ambao waliletwa Marekani na wazazi wao wakati wakiwa watoto.

Kiongozi huyo wa Marekani alizungumza wakati seneta mRepublican John McCain wa jimbo la Arizona na seneta mDemocrat Chris Coons wa jimbo la Delaware walipotoa pendekezo la kuwapatia kibali halali wahusika wa DACA mpango ulioanzishwa na utawala uliopita wa Rais Barack Obama ambao Rais Trump alikata kuongeza muda wa mpango huo utakao malizika mwezi ujao.

XS
SM
MD
LG