Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:00

Trump asema yeye sio mbaguzi


Vijana walioingizwa nchini kinyume cha sheria na wazazi wao wakionyesha mshikamano wao kushinikiza programu ya DACA iendelezwe.
Vijana walioingizwa nchini kinyume cha sheria na wazazi wao wakionyesha mshikamano wao kushinikiza programu ya DACA iendelezwe.

Rais Donald Trump amesema yeye sio mbaguzi Jumapili, siku tatu baada ya kuripotiwa kuwa amesema wahamiaji kutoka Haiti, El Salvador na Afrika wanatokea katika nchi alizozifananisha na choo.

“Mimi siyo mbaguzi kabisa ambaye utaweza kunihoji,” alijibu Trump swali la mwandishi katika Jumba lake la Kifahari huko Mar-a-Lago Florida lilioko ufukweni.

Trump amesema kuwa yuko tayari, anania na anauwezo wa kufikia makubaliano ya kuwahami wahamiaji vijana 800,000 wasiondolewe nchini Marekani, chini ya programu ya DACA, ambao miaka kadhaa iliyopita waliletwa na wazazi wao kinyume cha sheria nchini.

“Ukweli ni kuwa, sidhani kama Wademokrati wanataka kufikia makubaliano,” na mapema siku hiyo alisema anafikiria programu hiyo “huenda imeshakufa.”

Trump amedai kuwa wabunge wa chama cha Demokrat “hawataki kuwepo usalama katika mipaka, hawataki kuzuia madawa ya kulevya, wanataka kuondoa fedha kwenye bajeti ya jeshi kitu ambacho hatuwezi kufanya.” Katika ujumbe wake wa Twitter Jumatatu, Trump amesema, Marekani Kwanza na Tuifanye Marekani kuwa bora tena!”

Kauli mbaya inayodaiwa aliitoa Trump kuhusu watu wa Haiti, Salvador na wahamiaji kutoka Afrika imetikisa mazungumzo kuhusu kuwahami wahamiaji vijana kuondolewa chini ya programu ya kuchelewesha kwa muda kuchukuliwa hatua kuwaondoa vijana wanaoingia nchini (DACA) iliyokuwa imeanzishwa na Rais mstaafu Barack Obama.

Mazungumzo kati ya Ikulu ya White House na bunge la Marekani kuhusu programu ya DACA imefungamanishwa na mikutano ya dharura wiki hii juu ya kufadhili operesheni za serikali kuvuka saa sita ya usiku Ijumaa, wakati bajeti ya matumizi ya hivi sasa iliyoidhinishwa ikimalizika muda wake.

Kwa mujibu wa wale waliokuwepo katika ukumbi wa ikulu ya White House wakati wa mkutano huo juu ya wahamiaji wiki iliyopita, Trump alihoji ni kwa nini Marekani inaruhusu wahamiaji kutoka Haiti, El Salvador na Afrika na kusema anataka kuona wahiaji zaidi kutoka nchi kama vile Norway. Pia inavyoelekea ni kuwa anataka kuitoa Haiti katika mpango wa mageuzi ya wahamiaji.

Wakati ikulu ya White House haijakanusha kuwa Trump alitumia lugha chafu kuwaelezea wahamiaji ambao siyo wazungu, Trump alikanusha kwa ubabaishaji. “Lugha niliotumia wakati wa mkutano wa DACA ilikuwa mbaya, lakini hii siyo lugha iliyotumika,” amesema.

Siku ya Jumatatu, Josh Dawsey, mwandishi wa gazeti la The Washington Post aliyeibua habari kuhusu lugha chafu aliotumia Trump, akiwaambia shirika la habari la CNN kuwa maafisa wa ikulu ya White House wanasema kuwa inawezekana Trump alitoa tamko tofauti kidogo la matusi, akihoji ni kwa nini Marekani inawakubali wahamiaji kutoka nchi alizozifananisha na choo.

XS
SM
MD
LG