Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:53
VOA Direct Packages

Wakati vita kadhaa vikipamba moto nje ya nchi, shinikizo longezeka kwa Biden juu ya ahadi yake...


Wapalestina wakiwasalia ndugu zao waliouawa katika shambulizi la mabomu lililofanywa na Israeli katika Ukanda wa Gaza huko Deir al Balah, Oct.27, 2023. Picha na Shirika la habari la AP.
Wapalestina wakiwasalia ndugu zao waliouawa katika shambulizi la mabomu lililofanywa na Israeli katika Ukanda wa Gaza huko Deir al Balah, Oct.27, 2023. Picha na Shirika la habari la AP.

Kwa rais ambaye kampeni yake ilikuwa kumaliza “vita kabisa,” Joe Biden hivi sasa anakabiliwa na mgogoro wa Gaza ikiwa uko juu ya uvamizi wa Russia huko Ukraine na kuongezeka kwa mivutano kati ya China na Marekani juu ya Taiwan.

FILE PHOTO: Rais Joe Biden
FILE PHOTO: Rais Joe Biden

Wachambuzi wanaeleza kuwa jinsi atakavyo shughulikia hizi changamoto zinaweza kuwa na athari kwa azma yake ya kuchaguliwa tena mwaka 2024.

Athari za Mashambulizi ya anga ya Israeli

Katikati ya kuongezeka kwa vifo vya Wapalestina kutokana na mashambulizi ya anga ya Israeli ambayo Wizara ya Afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza inasema imevuka vifo 7,000, kuna tamko la Rais wa Marekani Joe Biden akisema:

Rais Joe Biden anaeleza: “Sina dhana ya kuwa Wapalestina wanasema ukweli kuhusu watu wangapi wameuawa. Nina hakika watu wasiokuwa na hatia wameuawa, na ni gharama inayolipwa kwa kuanzisha vita.”

Taarifa hiyo imewakasirisha Wamarekani wenye asili ya Kiarabu, Waislam na wengine ambao tayari wanaandama kukosoa jinsi Biden anavyo shughulikia vita vya huko Gaza.

Robert McCaw, wa Baraza la Mahusiano ya Marekani na Uislam anasema:

“Hili linashituwa sana na kuondoa ubinadamu. Je, rais atahisi vizuri iwapo watoto 1,000 tu wa Palestina watakufa.

Pia wale wenye msimamo wa kadri wanahasira. Wawakilishi tisa wa Bunge, wengi wao kutoka upande wa mrengo wa kati wa chama cha Demokratik cha Biden, walipiga kura dhidi ya azimio lililokuwa linaiunga mkono Israel na kulaani kikundi cha Hamas, kwa sababu lilikuwa haliombolezi vifo vya Wapalestina.

Tafiti mbali mbali za maoni zinaonyesha Wamarekani wengi zaidi wana masikitiko kwa Waisraeli kuliko Wapalestina, japokuwa Wamarekani vijana wamegawanyika katika hilo.

Larry Sabato, wa Kituo cha Siasa cha Chuo Kikuu cha Virginia anaeleza:

“Huku wa Wamarekani wenye asili ya kiyahudi, kikundi muhimu sana katika wapigaji kura na ambao wanatoa mchango mkubwa kwa Chama cha Demoratik, kumekuwa na pongezi za jumla za kimataifa kwa Rais Biden na jinsi alivyoshughulikia mgogoro wa Israel na Hamas.

Spika mpya wa Baraza la Wawakilishi Mike Johnson
Spika mpya wa Baraza la Wawakilishi Mike Johnson

Warepublikan katika Bunge wanaendeleza mashaka yao kuhusu ahadi ya Biden katika kufadhili vita vya nje.

Kati yao akiwemo Spika mpya wa Baraza la Wawakilishi aliyechaguliwa Mike Johnson, ambaye anaihurumia Israel lakini anapinga upelekaji fedha zaidi kwa Ukraine bila ya kuweka masharti.

Mwakilishi Mike Johnson, Spika wa Baraza hilo anasema:

“Mswaada wa kwanza ambao nitauleta ndani ya ukumbi katika kipindi kifupi kijacho itakuwa ni wakuwaunga mkono marafiki zetu wa karibu sana Israel. Na sisi tumechelewa kuchukua hatua.”

Idadi ya wapiga kura ambao wanakubaliana na Biden alivyoshughulikia suala hili la Israel imeongezeka kwa asilimia 9 tangu siku zilizofuatia shambulizi la Hamas ndani ya Israel.

Vipi vita vya huko Gaza vitaathiri kuchaguliwa tena kwa Biden katika kinyang’anyiro cha 2024 kutategemea iwapo vita hivyo vitaweza kudhibitiwa. Katika nchi jirani ya Lebanon, mashambulizi ya mpakani yameongezeka kati ya Israel na kikundi cha Hezbollah kinachoungwa mkono na Iran.

Larry Sabato anaeleza:

“Iwapo tutajiingiza kuhusika moja kwa moja na vita hivi vinavyoendelea daima, ndio, Biden atajikuta katika matatizo. Lakini kadiri atavyohakikisha majeshi ya Marekani hayako katika mapigano, Sifikirii kama kutakuwa na utatanishi. Sidhani itakuwa moja ya sababu kuu za watu kupiga kura.

Sabato ameongeza sababu nyingine kuu – iwapo vifo vya Wapalestina vitaweza kudhibitiwa, na misaada ya kibinadamu kufikishwa.

Ripoti ya Patsy Widakuswara, VOA News, White House.

Forum

XS
SM
MD
LG