Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:50

Wachambuzi wanaona mazoezi ya China na Russia ni ishara za kuimarisha ushirikiano kati yao


Mazoezi ya kijeshi ya pamoja kati ya China na Russia yanaendelea huko katika Bahari ya Japan.
Mazoezi ya kijeshi ya pamoja kati ya China na Russia yanaendelea huko katika Bahari ya Japan.

Wakati vita vya Ukraine vikiendelea, China na Russia wamefanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi katika Bahari ya Japan ambapo wachambuzi wanasema ni ishara za hivi karibuni za kuimarisha ushirikiano kati ya majeshi ya nchi mbili zenye nguvu duniani.

Mazoezi hayo pia ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na kuongezeka kwa ushirikiano wa Marekani na washirika wake katika eneo hilo, wameongeza kusema.

“Russia na China wanajaribu kupeleka ujumbe kwa Japan na Marekani kuwa hawafurahishwi kabisa ushirikiano wao katika NATO na eneo la [Indo-Pacific], na wanataka kuthibitisha kuwa wanaweza kufikia kiwango sawa vya ushirikiano kama huo katika eneo kama ilivyo kwa [Washington na washirika wake,] “ Stephen Nagy, mtaalam wa usalama wa kieneo katika Chuo Kikuu cha Christian, ameiambia VOA.

Kwa Russia, Nagy amesema, mazoezi hayo ni njia ya kuonyesha “kuwa wao bado wana uwezo wa kusimamia mizozo upande wa mashariki lakini pia wanaweza kujenga uwezo kwa eneo la Indo-Pacific kushirikiana na China na kuishinikiza Marekani.”

“Wanataka kuthibitisha kuwa bado wanaweza kushirikiana na China na kusababisha machafuko makubwa, hususan katika eneo la nyuma ya Japan,” alisema.

Siku ya Alhamisi, Waziri wa Ulinzi wa Russia alitangaza kuwa mazoezi ya “Northern/Interaction-2023” yalikuwa yameanza katika Bahari ya Japan na yatadumu hadi Jumapili Julai 23. Wizara hiyo ilisema kuwa zaidi ya urushaji wa makombora halisi, mazoezi hayo yatahusisha mazoezi ya “silaha za kuzamisha nyambizi na mashambulizi ya jeshi la majini”

Azma ya mazoezi hayo, wizara ya Russia ilisema, ni “kuimarisha ushirikiano wa jeshi la majini” kati ya nchi hizo mbili na “ kudumisha amani na utulivu katika eneo la Asia Pacific.” Russia na China zimesema wanapeleka manowari 10 na ndege za kivita 30 kushiriki katika zoezi hilo.

Kulingana na gazeti la serikali la Global Times, zoezi hili linaadhimisha kwa mara ya kwanza kwa jeshi la majini na la anga la Russia kushiriki katika mazoezi ya pamoja yanayoongozwa na China.

Mazoezi ya Northern/Interaction-2023 ni mazoezi ya kijeshi ya kwanza ya pamoja yaliyofanywa karibu na Japan mwaka huu, lakini kulingana na Taasisi ya Kimataifa ya utafiti wa kimkakati ( International Institute for Strategic Studies) Russia na China wamefanya angalau mazoezi ya kijeshi matano katika Bahari ya Japan na Bahari ya East China Sea mwaka uliopita.

Forum

XS
SM
MD
LG