Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 15:05

Putin aamua kutohudhuria mkutano wa BRICS


Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakiwa Saint Petersburg, Russia Juni 17, 2023. Picha na Reuters.
Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakiwa Saint Petersburg, Russia Juni 17, 2023. Picha na Reuters.

Rais wa Russia Vladimir Putin aliamua kutohudhuria mkutano wa BRICS utakaofanyika mjini Johannesburg kwa sababu hakutaka "kuhatarisha" mazungumzo hayo, mwanadiplomasia wa juu Afrika Kusini alisema Alhamisi.

Ziara hiyo muhimu kwa Putin iliiweka Afrika Kusini njia panda kidiplomasia na kisheria kabla ya mkutano kuanza tarehe 22 hadi 24 Agosti.

Putin ametolewa hati ya kukamatwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu(ICC) -- hatua ambayo Afrika Kusini kama mwanachama wa ICC ingetarajiwa kutekeleza agizo hilo iwapo Putin angeingia nchini humo.

Ofisi ya Rais Cyril Ramaphosa imemaliza hali ya sintofahamu siku ya Jumatano, na kutangaza kwamba Putin binafsi hatahudhuria mkutano huo, bali atawakilishwa na waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov.

Balozi wa Afrika Kusini kwa Asia na BRICS, Anil Sooklal, alisema kulingana na uamuzi "wa pamoja" uliofikiwa, Putin atashiriki majadiliano hayo kwa njia ya mtandao.

"Rais Putin anaelewa mkanganyiko ambao Afrika Kusini inakabiliana nao, lakini hakutaka kuuhatarisha mkutano huo, hakutaka kuleta matatizo kwa Afrika Kusini," Sooklal aliuambia mkutano wa vyombo vya habari mjini Johannesburg.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Rais Xi Jinping wa China na Rais Vladimir Putin wa Russia wakiwa Johannesburg, Julai 26 2018.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Rais Xi Jinping wa China na Rais Vladimir Putin wa Russia wakiwa Johannesburg, Julai 26 2018.

Pretoria ndiyo mwenyekiti wa sasa wa kundi la BRICS, kifupi cha mataifa yenye kiuchumi unaokuwa kwa kasi ya Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini, ambazo zinajiona kuwa ni mpinzani wa utawala wa kiuchumi wa nchi za Magharibi.

Afrika Kusini ilikuwa katika shinikizo kubwa la ndani na kimataifa la kutomkaribisha kiongozi wa Russia.

Sooklal alisema licha ya kutokuwepo kwa Putin serikali ina imani kuwa mazungumzo hayo "yatafanikiwa".

Kiongozi wa Russia "atashiriki kikamilifu katika majadiliano yote," kwa njia ya mtandao, alisema.

Putin anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa tuhuma za kuwafukuza kinyume cha sheria watoto wa Ukraine baada ya kumvamia jirani yake Februari 2022.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG