Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema Jumapili kuwa mkutano wa kilele wa mwezi ujao wa BRICS, ambao Vladimir Putin amealikwa kuhudhuria, utafanyika ana kwa ana licha ya hatiya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa Russia.
Afrika Kusini ni mwenyekiti wa sasa wa BRICS, kundi la ambalo linajumuisha Brazil, Russia, India na China kutoa changamoto kwa miundo ya utawala wa kimataifa unaoongozwa na Marekani na Ulaya.
Mkutano wa kilele wa BRICS unasonga mbele na tunakamilisha majadiliano yetu juu ya muundo, Ramaphosa aliwaambia waandishi wa habari wa Afrika Kusini, pembeni ya mkutano na chama tawala cha ANC, akiongeza kuwa utakuwa mkutano wa ana kwa ana.
Hakusema ikiwa Putin ambaye anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa tuhuma kwamba Russia iliwarudisha watoto wa Ukraine kinyume cha sheria, atahudhuria mkutano huo au la.
Forum