Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:17

Kumkamata Putin ni sawa na kutangaza vita dhidi ya Russia - Ramaphosa


Rais wa Urusi Vladimir Putin akipeana mkono na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa huko Saint Petersburg Russia, Juni 17, 2023. Picha na REUTERS.
Rais wa Urusi Vladimir Putin akipeana mkono na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa huko Saint Petersburg Russia, Juni 17, 2023. Picha na REUTERS.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa siku ya Jumanne kupitia barua aliyoandikia na kuwasilishwa mahakama amesema kwamba kukamatwa kwa rais wa Russia, Vladimiri Putin kunaweza kuwa sawa na kutangazwa kwa vita dhidi ya Russia.

Ramaphosa ameipitia barua hiyo wakati Afrika Kusini ikiendelea kutathmini namna ya kumpokea kiongozi huyo aliyealikwa kuhuduria mkutano wa viongozi wa BRICS utakaofanyikia mjini Johanesburg mwezi ujao.

Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa, ICC imetoa hati ya kukamatwa kwa rais huyo wa Russia, na hivyo, kwa vile Afrika Kusini ni mwanachama wa mahakama hiyo, inabidi kusaidia kukamatwa kwake endapo atahudhuria mkutano huo.

Mvutano huo wa kidiplomasia unaohusiana na suala hilo unajitokeza mbele ya mahakama ya Afrika Kusini, ambako chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance, DA kinajaribu kuishinikiza serikali kumkamata na kukabidhi Putin kwa mahakama ya ICC, endapo ataingia nchini humo.

Hata hivyo Ramaphosa kupitia barua hiyo aliyopeleka mahakamani ameeleza kwamba ombi la chama hicho halistahiki na linahatarisha usalama wa taifa.

Ramaphosa amesema kwamba Russia imeweka wazi kwamba kukamatwa kwa kiongozi wake ni sawa na kutangaza vita dhidi ya taifa hilo. Na kuongeza kuwa ni kinyume cha sheria na kunahatarisha kuingia kwenye vita na Russia, na pia ni kinyume na jukumu lake la kulinda taifa.

Afrika kusini ambayo ni mwenyekiti wa sasa wa Brics, ambayo inazijumuisha Brazil, Russia, India na China na kuchukuliwa kama chombo kikuu cha upinzani wa kiuchumi dhidi nya nchi za magharibi.

Forum

XS
SM
MD
LG