Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:17

Viongozi wa mataifa jirani na Sudan wakutana Misri, wahimiza usitishwaji wa mapigano


Mkutano wa viongozi wa mataifa jirani na Sudan, Cairo, Julai 13, 2023
Mkutano wa viongozi wa mataifa jirani na Sudan, Cairo, Julai 13, 2023

Mkutano wa viongozi wa Afrika kutoka mataifa jirani na Sudan, inayokumbwa na vita, Alhamisi umehimiza kusitishwa kwa mapigano, huku wataalamu wa Umoja wa mataifa wakiripoti kuwa kaburi la watu wengi limegunduliwa katika jimbo la Darfur nchini humo.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) imesema imeanzisha uchunguzi mpya kuhusu madai ya uhalifu wa kivita nchini Sudan, na kuongeza kuwa kuongezeka kwa ghasia ni “jambo linalotia wasiwasi mkubwa”.

Huku Misri ikiwa mwenyeji wa mkutano huo kuhusu mzozo uliodumu kwa takriban miezi mitatu, mapigano ya silaha, milipuko na mingurumo ya ndege za kivita iliutikisa tena mji mkuu wa Sudan, Khartoum, wakazi wameliambia shirika la habari la AFP.

Watu 3,000 wameuawa na mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao kufuatia vita hivyo kati ya majenerali hasimu, kulingana na shirika lisilo la kiserikali linalofuatilia migogoro (ACLED).

Viongozi wa Misri, Ethiopia, Eritrea, Chad, Sudan Kusini, Jamhuri ya Afrika ya kati na Libya, vile vile Umoja wa Afrika na Jumuia ya nchi za kiarabu walikutana mjini Cairo kujadili vita hivyo na athari zake kwa nchi jirani.

Umoja wa mataifa ulionya kwamba kuna hatari mzozo wa Sudan ukageuka “vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe, vinavyoweza kuyumbisha usalama wa eneo lote.”

Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Karim Khan alisema katika ripoti kwa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa Alhamisi kwamba ofisi yake “inaweza kuthibitisha kwamba imeanzisha uchunguzi kuhusiana na matukio yanayoendelea katika mazingira ya mapigano ya sasa.”

Khan alisema kumekuwa na “mawasiliano mbalimbali” kuhusu madai ya uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini Sudan tangu mapigano yalipozuka mwezi Aprili.

Forum

XS
SM
MD
LG