Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:46

Jacob Zuma anakabiliwa na sintofahamu ya kurudi gerezani, aliachiliwa kinyume cha sheria


Aliyekuwa rais wa Afrika kusini Jacob Zuma
Aliyekuwa rais wa Afrika kusini Jacob Zuma

Mahakama ya katiba nchini Afrika Kusini imetoa maamuzi kuwa kuachiliwa mapema kwa rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma kutoka gerezani kwa madai kwamba alikuwa anakumbana na matatizo ya kiafya, ni hatua iliyotekelezwa kinyume cha sheria.

Zuma aliachiliwa kutoka gerezani mwaka 2021, chini ya wiki nane baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi 15 gerezani kwa kukiuka amri ya mahakama.

Hukumu dhidi ya Zuma ilitolewa baada ya yake kukataa kutoa ushahidi katika kesi dhidi ya ufisadi iliyotokea wakati alipokuwa ofisini.

Ombi la kutaka kuachiliwa huru kwa sababu za kiafya lilikubaliwa na idara ya magereza. Ombi hilo liliwasilishwa na Arthur Fraser, mwenye uhusiano wa karibu sana na rais huyo wa zamani.

Haijabainika iwapo Zuma ataamriwa kurudi gerezani kufuatia uamuzi huo.

Zaidi ya watu 300 walifariki katika maandamano yaliyotokea baada ya Zuma kukamatwa.

Forum

XS
SM
MD
LG