Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 02:02

Putin kutohudhuria mkutano wa BRICS Afrika Kusini


Rais wa Russia, ambaye yupo matatani baada ya kutolewa hati ya kukamatwa, hata hudhuria mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, mwezi ujao, rais wa nchi hiyo amesema Jumatano, na kumaliza tetesi kama rais wa Russia, atahudhuria.

Uwezekano wa rais Putin, kuhudhuria mkutano huo ulizusha mgongano wa kidiplomasia mjini Pretoria.

Kiongozi wa Russia, anatakiwa kukamatwa na mahakama ya kimataifa baada ya hati kutolewa, ambapo Afrika Kusini kutokana kuwa mwanachama wa mahakama hiyo ilipaswa kuwajibika kwa kumkamata kiongozi huyo pale tu atakapotua nchini humo.

Katika taarifa msemaji wa rais wa Afrika Kusini, Vincent Mangwenya, alieleza kuwa rais Cyril Ramaphosa, amesema kwamba kutokana na makubaliano ya pande zote, rais Vladimir Putin, wa shirikisho la Russia, hato hudhuria kikao.

Uamuzi huo umefikiwa bada ya mashauriano kadhaa yaliyofanywa na Ramaphosa hivi karibuni ambayo ya karibuni kabisa yamefanyika jana usiku.

Forum

XS
SM
MD
LG